Imesasishwa Januari 2, 2026.
Veriafya inatambua na kuheshimu haki ya faragha ya kila mtumiaji wa tovuti na majukwaa yake ya kidijitali. Sera hii ya Faragha inaeleza namna Veriafya inavyokusanya, kutumia, kuhifadhi na kulinda taarifa binafsi, pamoja na haki na wajibu wa mtumiaji anapotumia huduma zetu. Kwa kuendelea kutumia Veriafya, mtumiaji anakiri kuwa amesoma, ameielewa na amekubali masharti ya sera hii.
Hatutibu, tunatoa elimu
Veriafya ni jukwaa la mawasiliano ya afya linalotoa elimu ya afya na taarifa zilizohakikiwa kwa madhumuni ya kielimu pekee. Maudhui yote yanayotolewa hayakusudiwi kuchukua nafasi ya ushauri, uchunguzi au matibabu ya kitaalamu yanayotolewa na mtaalamu wa afya aliyesajiliwa. Mtumiaji anabeba jukumu la kutafuta ushauri wa kitaalamu kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusiana na afya yake.
Katika matumizi ya kawaida ya tovuti au huduma zetu, Veriafya inaweza kukusanya taarifa binafsi pale mtumiaji anapozitoa kwa hiari, ikiwemo jina, barua pepe, ujumbe, maoni au maswali yanayowasilishwa kwa madhumuni ya mawasiliano au uhakiki wa taarifa. Aidha, taarifa fulani hukusanywa kiotomatiki, kama vile aina ya kifaa, kivinjari kinachotumika, kurasa zinazotembelewa na muda wa matumizi, kwa lengo la kuboresha utendaji na usalama wa tovuti.
Tunatumia vidakuzi
Veriafya hutumia vidakuzi (cookies) na teknolojia zinazofanana ili kuchambua mwenendo wa matumizi, kuboresha uzoefu wa mtumiaji na kuhakikisha tovuti inafanya kazi kwa ufanisi. Mtumiaji ana hiari ya kudhibiti au kuzima matumizi ya cookies kupitia mipangilio ya kivinjari chake, ingawa kufanya hivyo kunaweza kuathiri upatikanaji wa baadhi ya huduma.
Taarifa binafsi zinazokusanywa hutumika kwa misingi halali ya kisheria, ikiwemo ridhaa ya mtumiaji, utekelezaji wa huduma zilizoombwa, kutimiza wajibu wa kisheria, pamoja na maslahi halali ya Veriafya katika kuendesha, kulinda na kuboresha huduma zake. Taarifa hizo hutumika kuboresha maudhui, kujibu mawasiliano, kufanya uchambuzi wa matumizi na kuhakikisha usalama wa mifumo yetu.
Tunalinda taarifa zako
Taarifa binafsi zitahifadhiwa kwa muda unaohitajika tu kutimiza madhumuni yaliyokusudiwa au kwa mujibu wa matakwa ya sheria zinazotumika. Veriafya huchukua hatua stahiki za kiufundi, kiutawala na kimfumo kulinda taarifa dhidi ya upotevu, ufikiaji usioidhinishwa au matumizi mabaya, ingawa inatambuliwa kuwa hakuna mfumo wa kidijitali ulio salama kwa asilimia mia moja.
Kwa mujibu wa sheria husika, mtumiaji ana haki ya kuomba ufikiaji wa taarifa zake binafsi, kuomba marekebisho au kufutwa kwa taarifa hizo, au kuondoa ridhaa aliyotoa awali. Maombi yote yanayohusiana na haki za faragha yawasilishwe kupitia mawasiliano rasmi ya Veriafya.
Veriafya ina haki ya kufanya marekebisho ya sera hii ya Faragha wakati wowote. Marekebisho yataanza kutumika mara tu yatakapochapishwa kwenye tovuti, na mtumiaji anahimizwa kupitia sera hii mara kwa mara ili kufahamu mabadiliko yoyote.
Sera hii ya Faragha itaongozwa na kutafsiriwa kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa maswali, maoni au malalamiko yanayohusiana na faragha au matumizi ya taarifa binafsi, tafadhali wasiliana nasi kupitia mawasiliano rasmi ya Veriafya.
Mawasiliano
Barua pepe: office@veriafya.org
Tovuti: www.veriafya.org
Kwa kutumia huduma za Veriafya, mtumiaji anakubali kuwa sera hii ni sehemu ya masharti ya matumizi ya Jukwaa.
