{"id":4471,"date":"2021-06-20T07:09:00","date_gmt":"2021-06-20T07:09:00","guid":{"rendered":"https:\/\/afyainfo.co.tz\/?p=4471"},"modified":"2025-01-02T17:41:40","modified_gmt":"2025-01-02T17:41:40","slug":"vernix-caseosa-faida-kwa-mtoto","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/veriafya.org\/?p=4471","title":{"rendered":"UHALISIA: Utando Mweupe (Vernix) Anaozaliwa nao Mtoto si Shahawa"},"content":{"rendered":"<p class=\"p1\"><span class=\"s1\">Vernix ni utando mweupe unaotengenezwa kwenye ngozi ya mtoto kwenye kipindi cha mwisho cha ujauzito.<\/span><\/p>\n<p class=\"p1\"><span class=\"s1\">Huundwa na maji kwa asilimia 80, mafuta kwa asilimia 10 na protini kwa asilimia 10. (<a href=\"https:\/\/obgyn.onlinelibrary.wiley.com\/doi\/abs\/10.1111\/jog.14103\">1<\/a>)<\/span><\/p>\n<p class=\"p1\"><span class=\"s1\">Utando huu kwa nyakati nyingi umekuwa chanzo cha unyanyasaji kwa wanawake kutokana na uwepo wa dhana potofu tatu ambazo ni mwanamke mjamzito kushiriki tendo la ndoa\u00a0hadi siku za karibu kabisa za kujifungua, kuzini nje ya ndoa pamoja na mwanamke kupenda kula aina fulani ya vyakula na vinywaji wakati wote wa ujauzito.<\/span><\/p>\n<h2 class=\"p1\"><strong><span class=\"s1\">Uhalisia<\/span><\/strong><\/h2>\n<p class=\"p1\"><span class=\"s1\">Dhana zote hizi hazina ukweli wowote.<\/span><\/p>\n<p class=\"p1\"><span class=\"s1\">Tofauti na jinsi inavyoaminika mitaani, utando huu hautokani na matumizi ya aina fulani ya chakula au kinywaji, kuzini, uwepo wa ugonjwa au hata mama mjamzito kushiriki tendo la ndoa hasa siku za mwisho kabisa za ujauzito wake.<\/span><\/p>\n<p class=\"p1\"><span class=\"s1\">Watoto waliozaliwa wakati sahihi huwa na kiasi kikubwa cha utando huu huku waliozaliwa kwa kupitiliza siku zao wakizaliwa na utando kidogo sana. (<a href=\"https:\/\/onlinelibrary.wiley.com\/doi\/full\/10.1111\/j.1467-2494.2006.00338.x\">2<\/a>,<a href=\"https:\/\/journals.plos.org\/plosone\/article?id=10.1371\/journal.pone.0099173\">3<\/a>,<a href=\"https:\/\/www.ncbi.nlm.nih.gov\/pmc\/articles\/PMC2763724\/\">4<\/a>)<\/span><\/p>\n<p><span class=\"s1\">Vernix siyo shahawa, wala haina uhusiano wowote na kitu hicho<\/span><\/p>\n<h2 class=\"p1\"><strong><span class=\"s1\">Kazi Z<\/span><\/strong><span class=\"s1\">ake<\/span><\/h2>\n<p class=\"p1\"><span class=\"s1\">Vernix caseosa hufanya mambo kazi kuu 5 ambazo ni;<\/span><\/p>\n<ul class=\"ul1\">\n<li class=\"li1\"><span class=\"s1\">Kuzuia maambukizi ya magonjwa ya ngozi kwa watoto wakati akiwa tumboni na baada ya kuzaliwa.<\/span><\/li>\n<li class=\"li1\"><span class=\"s1\">Kupunguza msuguano kati ya mama na mtoto wakati wa kujifungua.<\/span><\/li>\n<li class=\"li1\"><span class=\"s1\">Kutunza joto bora kabisa linalofaa kwa ajili ya ukuaji wa siku za mwanzo za mtoto.<\/span><\/li>\n<li class=\"li1\"><span class=\"s1\">Kuipatia ngozi ya mtoto unyevu unaostahili.<\/span><\/li>\n<li class=\"li1\"><span class=\"s1\">Kuzuia ngozi ya mtoto isiharibike na mabadiliko ya hali ya hewa.<\/span><\/li>\n<\/ul>\n<p class=\"p1\"><span class=\"s1\">Kwa kuwa mtoto huelea kwenye mfuko wa uzazi uliojaa maji (maji ya uzazi) kwa miezi mingi sana, huwa ni lazima utando huu utengenezwe ili kuilinda ngozi ya mtoto kwanza akiwa bado anaelea tumboni kisha baada ya kuzaliwa. (<a href=\"https:\/\/www.ncbi.nlm.nih.gov\/books\/NBK559238\/\">5<\/a>,<a href=\"https:\/\/www.nature.com\/articles\/pr2007169\">6<\/a>,<a href=\"https:\/\/www.karger.com\/Article\/Abstract\/328744\">7<\/a>,<a href=\"https:\/\/www.jcdr.net\/article_fulltext.asp?id=6784\">8<\/a>)<\/span><\/p>\n<h2 class=\"p1\"><span class=\"s1\">Kuoga<\/span><\/h2>\n<p class=\"p1\"><span class=\"s1\">Hakuna sheria inayolazimisha kumuosha mtoto moja kwa moja baada tu ya kuzaliwa na kuukwangua uchafu huu.<\/span><\/p>\n<p class=\"p1\"><span class=\"s1\">Kumuacha mtoto na utando huu kwa muda kidogo kabla ya kumuogesha huwa na faida nyingi kwa afya yake.<\/span><\/p>\n<p class=\"p1\"><span class=\"s1\">Mtoto anaweza tu kufutwa kwa kitambaa kisafi ili kuondoa damu iliyomchafua wakati wa kuzaliwa. (<a href=\"https:\/\/bmcresnotes.biomedcentral.com\/articles\/10.1186\/s13104-020-05282-0\">9<\/a>,<a href=\"https:\/\/www.jognn.org\/article\/S0884-2175(18)30125-4\/fulltext\">10<\/a>)<\/span><\/p>\n<p class=\"p1\"><span class=\"s1\">Wauguzi huwatenganisha watoto na mama zao baada tu ya kujifungua kwa ajili ya uchunguzi na usafi (kumuogesha).<\/span><\/p>\n<p class=\"p1\"><span class=\"s1\">Uchunguzi ni jambo la muhimu na lazima, lakini kumuogesha mtoto siyo lazima. Unaweza kuamua mwenyewe mtoto aogeshwe lini kwa mara ya kwanza.<\/span><\/p>\n<h2 class=\"p1\"><span class=\"s1\">Ushauri<\/span><\/h2>\n<p class=\"p1\"><span class=\"s1\">Shirika la Afya Duniani (WHO) hushauri kusubiri walau kwa <a href=\"https:\/\/www.who.int\/tools\/your-life-your-health\/life-phase\/newborns-and-children-under-5-years\/caring-for-newborns\">saa 24<\/a> ndipo mtoto aogeshwe kwa mara ya kwanza.<\/span><\/p>\n<p class=\"p1\"><span class=\"s1\">Hata hivyo, umuhimu wa kuchelewa kumuogesha mtoto hupungua hasa ikiwa ngozi yake imechangangikana na choo chake cha kwanza.<\/span><\/p>\n<p class=\"p1\"><span class=\"s1\">Katika mazingira haya, kumuogesha mtoto mapema tu baada ya kuzaliwa kwake huwa ni jambo la lazima.<\/span><\/p>\n<p class=\"p1\"><span class=\"s1\">Kutokana na umuhimu wa utando huu pamoja na mazingira halisi yanayo zunguka utengenezwaji wake, ni wazi kuwa mwanamke amekuwa mhanga wa jambo lililo nje ya uwezo wake kwa muda mrefu.<\/span><\/p>\n<p class=\"p1\"><span class=\"s1\">Sasa ni muda sahihi wa kuacha kuwanyanyasa na kuwatuhumu kwa mambo ambayo hayana ukweli wowote.<\/span><\/p>\n<p class=\"p1\"><span class=\"s1\">Badala ya kuendelea kuelekeza mzigo wa lawama kwa wanawake, ni muhimu sasa kwa jamii nzima kujifunza na kufahamu umuhimu wa utando huu kwa afya za watoto.\u00a0<\/span><\/p>\n","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>Vernix ni utando mweupe unaotengenezwa kwenye ngozi ya mtoto kwenye kipindi cha mwisho cha ujauzito. Huundwa na maji kwa asilimia 80, mafuta kwa asilimia 10 na protini kwa asilimia 10. (1) Utando huu kwa nyakati nyingi umekuwa chanzo cha unyanyasaji kwa wanawake kutokana na uwepo wa dhana potofu tatu ambazo ni mwanamke mjamzito kushiriki tendo [&hellip;]<\/p>\n","protected":false},"author":1,"featured_media":6017,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[97],"tags":[112,113,114],"class_list":["post-4471","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","category-uhalisia","tag-uchafu-mweupe","tag-utando-si-shahawa","tag-vernix-caseosa"],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/veriafya.org\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/4471","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/veriafya.org\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/veriafya.org\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/veriafya.org\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/users\/1"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/veriafya.org\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcomments&post=4471"}],"version-history":[{"count":2,"href":"https:\/\/veriafya.org\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/4471\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":13756,"href":"https:\/\/veriafya.org\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/posts\/4471\/revisions\/13756"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/veriafya.org\/index.php?rest_route=\/wp\/v2\/media\/6017"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/veriafya.org\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fmedia&parent=4471"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/veriafya.org\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Fcategories&post=4471"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/veriafya.org\/index.php?rest_route=%2Fwp%2Fv2%2Ftags&post=4471"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}